Klabu
ya Bongo Movie Unity imedaiwa kuingia kwenye mpasuko mkubwa baada ya
baadhi ya viongozi kutangaza kuachia ngazi kwa madai ya kuwa mwenyekiti
wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amechikichia mtonyo (fedha) mwingi
wa klabu kwa masilahi yake
Kwa
mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya klabu hiyo, juzikati viongozi
wote wa klabu hiyo walikaa kikao kilichoitishwa na katibu wao, William
Mtitu ambacho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kumwajibisha Steve
Nyerere kwa madai hayo.
“Kuna fedha zilikuwa ni za maandalizi kwa ajili ya dua ya wasanii waliofariki dunia iliyofanyika Jumamosi.
“Pia kuna fedha nyingine zilitolewa hivi karibuni, walizitafuna akina Steve na baadhi ya viongozi, kilinuka kishenzi,” kilisema chanzo.
Imeelezwa
kuwa katika kikao hicho, hawakufikia muafaka kwani mtuhumiwa (Steve
Nyerere) hakutokea pasipo kujulikana sababu za kutofika kwake.
Chanzo
kiliendelea kudai, baada ya Steve kutoonekana, baadhi ya viongozi
walisusa na kuondoka ambapo Katibu Msaidizi wa Bongo Movie, Devotha
Mbaga na Mwekahazina Msaidizi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ walitangaza kuachia
ngazi endapo muafaka wa fedha zinazodaiwa kuliwa kinyemela
hautapatikana.
“Bongo
Movie ni kivumbi mtindo mmoja kwa sababu baadhi ya viongozi walio
karibu na Steve wanadaiwa kuchikichia fedha nyingi tu, kitu ambacho
kinazua mtafaruku kwani siyo mara ya kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Mtitu
ambaye ni katibu wa klabu hiyo, alipohojiwa kuhusiana na ishu hiyo,
alikiri kutokea ambapo alisema hata yeye amejipanga kuachia ngazi endapo
hatapewa ufafanuzi wa fedha zinazodaiwa kuliwa na mwenyekiti wao.
0 comments:
Post a Comment