Shirika la kutetea haki za
binadamu la Human Rights Watch limewalaumu polisi wa kupamba na ugaidi
nchini Kenya kwa kufanya mauaji ya kiholela.
Human Rights Watch inasema kuwa pia imepata
ushahidi wa watu kutoweka kwa lazima, kushikwa bila sababu na
kudhulumiwa kwa washukiwa.Shirika hilo pia linasema kuwa watoa misaada wa kimataifa wanastahili kusitisha misaada yao kwa polisi wa kupambana na na ugaidi kikosi kilichobuniwa baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa marekani mjini Nairobi mwaka 1998
0 comments:
Post a Comment