Serikali imeombwa kupeleka haraka vifaa vyenye uwezo wa kuwatambua watu wenye maambukizi ya ugonjwa wa ebola katika mpaka wa Tanzania na Zambia mjini Tunduma ili kuepusha ugonjwa huo kuingia nchini kirahisi kwa kupitia katika mpaka huo.
Mpaka huo unatumiwa na nchi zaidi ya sita za Kusini mwa Afrika.
Ombi hilo lilitolewa na baadhi ya wakazi wa mji wa Tunduma wakati wakizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki kuhusiana na tahadhari inayoweza kuchukuliwa ili kuepusha ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuenea katika nchi za Afrika Magharibi kuingia nchini.
Wananchi hao pia wameitaka serikali kuanza kutoa elimu kwa wananchi wanaoshi maeneo ya mipakani juu ya dalili za ugonjwa huo ili iwe rahisi kwao kujikinga na kutoa taarifa punde wanapomuona mtu mwenye dalili za kuugua ugonjwa huo.
Diwani wa Kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka, alisema kuwa hadi sasa, hakuna elimu iliyotolewa kwa wananchi juu ya ugonjwa huo wala tahadhari iliyochukuliwa na serikali kwa wageni wanaoingia nchini kupitia mpaka wa Tunduma.
“Mpaka sasa hakuna jitihada zozote zilizofanywa na serikali kuwakinga Watanzania wasipatwe na maambukizi ya ebola kutoka kwa wageni wanaoingia nchini kupitia mpaka huu," alisema.
Naye Samwel Mkisi, mkazi wa Tunduma, alisema ugonjwa huo wanausikia tu kupitia kwenye vyombo vya habari.
Kaimu Ofisa Afya katika mpaka wa Tunduma, Jamal Mohamed, alisema kazi ya kuwapima wageni wanaoingia na kutoka ili kutambua kama wana maambukizi ya ebola, bado haijaanza kutokana na kutokuwapo kwa vifaa.
Hata hivyo, alisema kuwa tayari serikali imevituma vifaa hivyo kutoka Dar es Salaam na kwamba kazi ya upimaji itaanza mara moja.
Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mipakani mkoani Mbeya ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji, Lusarago Mleka, alisema kutokana na kutokuwapo kwa udhibiti wa kiafya, kunasababisha watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kwa hofu
0 comments:
Post a Comment