Rais wa Marekani Barack Obama
amesema majeshi ya Iraq na yale ya Kikurd yamepiga hatua kubwa kulitwaa
tena bwawa muhimu la Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu kaskazini
mwa Iraq.
Amesema wamethibitisha kwamba wanauwezo wa
kufanya kazi kwa pamoja na wataendelea kuungwa mkono na majeshi ya
Marekani, ambayo tayari yamefanya mashambulio Zaidi ya anga katika eneo
linalokaliwa na wapiganaji wa kiislamu.Katika hatua nyingine kundi la himaya ya kiislamu linalofanya mashambulizi dhidi ya Wakurd limekanusha kwamba wapiganaji wake wamepoteza udhibiti wa bwawa hilo.
Wakati huohuo kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amesema jumuia ya kimataifa itakuwa na haki katika kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo hao .
Papa Amesema ni halali kuzuia kile alichokiita dhuluma ya kichokozi. Lakini ametahadharisha kuwa hatua yoyote itakayochukuliwa lazima ifanyiwe tathmini. kusimamisha na kwamba hakusema. Mwandishi wa BBC MJINI Roma Italia anasema papa Fransis hajaonesha kuunga mkono mashambulio ya anga yanayofanywa hivi sasa na Marekani dhidi ya wapiganaji hao wa kiislamu
0 comments:
Post a Comment