Ofisa mmoja mwanamke mwenye cheo
cha juu katika bank kubwa iliyoko mjini Kuala Lumpur , Malaysia pamoja
na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka
katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia
Air Line MH370 ambayo ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika
bahari ya Hindi mapema mwezi March.
Pamoja na kushtakiwa huko, mtu na mkewe hao
waliepuka makosa mengine yapatayo 16 kati ya makosa hayo yamo
wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kupoka pesa.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia
0 comments:
Post a Comment