Msanii wa Hip Hop kutokea Mwanza, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amesema kuwa majanga anayopata kwenye mahusiano yake yanatokana na kutompata mwanamke anayemhitaji.
Akizungumza na Mkasi TV hivi karibuni, Dudu Baya amesema wanawake wengi anaokutana naowanakuwa ni machizi. “Kwanza sijabahatika kukutana na mwanake ambae mimi namtaka, nafikiri Mungu bado hajanipa huwaga nakutana na machizi, kwa sababu mimi sipendi, mwanamke aliyelelewa na kufundwa vizuri vitu vya ndani huwezi ukavitoa nje.
Kwa
mimi binafsi siongeagi kwa wanaume wengine, napenda sana siri za
familia zibaki kuwa siri za familia. Kwa mfano huyu jinsi alivyoenda
kwenye media asitarajie nimtamrudia kabisa, ile tabia ya kwenda kwa
jirani na kanga moja ikianguka? Kweli kabisa kicheni party zinaendelea
lakini hazisaidii kitu chochote,” alisema
0 comments:
Post a Comment