#Category 1

Browse More

#Category 2

Browse More

#Category 3

Browse More

#Category 4

Browse More

Wednesday, 20 August 2014

Marekani yalaani mauaji ya mwandishi

James Foley
Rais Barack Obama wa Marekani amesema mauaji ya mwandishi wa habari James Foley raia wa Marekani aliyeuawa na wapiganaji wa kundi la Kiislam yameishtua dunia.
Obama amesema kitendo hicho ni cha kikatili na kisichokubalika mbele za Mungu na kwamba ni matokeo ya mawazo duni yasiyoendana na karne ya sasa.
Kauli hiyo ya Rais Obama inakuja huku wazazi wa mwandishi huyo wakielezea kutoridhishwa kwao na hatua zinazochukuliwa na Marekani kutokana na mauaji ya mtoto wao.
Wazazi hao wamesema wakati mwingine waandishi wa habari huru hawathaminiwi katika aki zao hata pale wanapojitolea maisha yao kwa ujira mdogo

Kufa Kufaana

Ndege ya shirika la ndege ya malaysia wakati wa uhai wake.
Ofisa mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyoko mjini Kuala Lumpur , Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia Air Line MH370 ambayo ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika bahari ya Hindi mapema mwezi March.
Pamoja na kushtakiwa huko, mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine yapatayo 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo.
Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kupoka pesa.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia

Maporomoko ya ardhi yaua watu 32 Japan

Maporomoko ya ardhi Japan
Watu wapatao 32 wameuawa katika maporomoko ya ardhi katika mkoa wa Hiroshima nchini Japan.
Maporomoko ya ardhi yametokea katika eneo la makaazi ya watu karibu na mlima katika vitongoji vya mji wa Hiroshima.
Maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwa saa 24 kuamkia Jumatano asubuhi zikiwa sawa na kipimo cha mvua za mwezi mzima, limesema Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Japan.
Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha nyumba zikiwa zimefukiwa katika matope na miamba, wakati kikosi cha uokoaji kikielekea nyumba hizo.
Watu wengine tisa bado hawajulikani walipo, limesema shirika hilo.
Afisa mwingine wa serikali ya mtaa katika mji huo amesema "baadhi ya watu wamechukuliwa na maji na ilikuwa vigumu kujua kwa uhakika idadi yao", Shirika la habari la AP limesema.
Mwandishi wa habari wa BBC Rupert Wingfield-Hayes amesema wengi wa waliokufa ni watoto.
Mmoja mwenye umri mdogo kabisa kufariki dunia katika tukio hilo ni mvulana mwenye umri wa miaka miwili, Shirika la habari la Japan, Kyodo limeripoti.
Miongoni mwa waliokufa ni mfanyakazi wa uokoaji mwenye umri wa miaka 53 ambaye amekufa baada ya udongo kuporomoka tena, shirika la Hali ya Hewa la Japan limesema. Aliweza kuwaokoa watu watano wakati wa operesheni hiyo.
Maporomoko hayo yamelikumba eneo la makaazi nje kidogo ya mji wa Hiroshima magharibi mwa Japan
Mtu mmoja akiwa amesimama katika kifusi cha nyumba katika kisiwa cha Izu Oshima kusini mwa Tokyo Oktoba 16,2013
Matope na miamba ilizikumba nyumba kadha, na kuwaacha wakijihifadhi kwenye mapaa ya nyumba.
Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta watu walionusurika lakini haijafahamika ni watu wangapi wamepotea.
Mmoja wa walionusurika ameliambia shirika la AP: "Niliamka katikati ya usiku na njia ya sehemu ya kuelekea chumba cha maongezi ilikuwa tayari imefurika maji."
"nilisikia sauti ya maji yakiingia, na hatimaye maji kutoka mtoni yaliingia ndani ya nyumba yangu, kwa hiyo nilichukua gari na kuondoka."
Profesa mmoja katika chuo kikuu cha Hiroshima, JJ Walsh, ameiambia BBC kila mtu alishangazwa na kiwango cha upepo huo.
"Watu wengi wamezoea mvua kubwa. Tuna msimu wa mvua. Lakini nafikiri kila mtu alikutwa na hali hii bila kujitayarisha kwa kiwango cha mvua iliyonyesha," amesema.
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amewataka maafisa wa serikali katika eneo hilo kuongeza idadi ya wafanyakazi wa uokoaji ili kuimarisha operesheni ya uokoaji".
Mvua zaidi zinaweza kusababisha maporomoko zaidi ya ardhi, wameonya maafisa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.
Sehemu kubwa ya sehemu ya kati na kusini mwa Japan ni milima, huku nyumba nyingi zikiwa zimejengwa katika miteremko mikali.
Mwaka uliopita, kimbunga kilisababisha maporomoko ya ardhi katika kisiwa cha Izu Oshima, kusini mwa mji mkuu wa Tokyo, ambapo watu 35 walikufa

Tuesday, 19 August 2014

Steve nyerere adaiwa kuingia mitini na Mikwanja ya Bongo Muvi


Klabu ya Bongo Movie Unity imedaiwa kuingia kwenye mpasuko mkubwa baada ya baadhi ya viongozi kutangaza kuachia ngazi kwa madai ya kuwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amechikichia mtonyo (fedha) mwingi wa klabu kwa masilahi yake
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya klabu hiyo, juzikati viongozi wote wa klabu hiyo walikaa kikao kilichoitishwa na katibu wao, William Mtitu ambacho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kumwajibisha Steve Nyerere kwa madai hayo.
“Kuna fedha zilikuwa ni za maandalizi kwa ajili ya dua ya wasanii waliofariki dunia iliyofanyika Jumamosi.
 
“Pia kuna fedha nyingine zilitolewa hivi karibuni, walizitafuna akina Steve na baadhi ya viongozi, kilinuka kishenzi,” kilisema chanzo.
Imeelezwa kuwa katika kikao hicho, hawakufikia muafaka kwani mtuhumiwa (Steve Nyerere) hakutokea pasipo kujulikana sababu za kutofika kwake.
Chanzo kiliendelea kudai, baada ya Steve kutoonekana, baadhi ya viongozi walisusa na kuondoka ambapo Katibu Msaidizi wa Bongo Movie, Devotha Mbaga na Mwekahazina Msaidizi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ walitangaza kuachia ngazi endapo muafaka wa fedha zinazodaiwa kuliwa kinyemela hautapatikana.
“Bongo Movie ni kivumbi mtindo mmoja kwa sababu baadhi ya viongozi walio karibu na Steve wanadaiwa kuchikichia fedha nyingi tu, kitu ambacho kinazua mtafaruku kwani siyo mara ya kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Mtitu ambaye ni katibu wa klabu hiyo, alipohojiwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kutokea ambapo alisema hata yeye amejipanga kuachia ngazi endapo hatapewa ufafanuzi wa fedha zinazodaiwa kuliwa na mwenyekiti wao.
Steve Nyerere alipopigiwa simu kwa lengo la kuulizwa juu ya madai hayo, simu yake iliita bila majibu. Jitihada za kumtafuta zinaendelea

Dudu Baya: Sijabahatika kumpata mwanamke ninayemtaka, nakutana na machizi

 Msanii wa Hip Hop kutokea Mwanza, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amesema kuwa majanga anayopata kwenye mahusiano yake yanatokana na kutompata mwanamke anayemhitaji.

 Akizungumza na Mkasi TV hivi karibuni, Dudu Baya amesema wanawake wengi anaokutana naowanakuwa ni machizi. “Kwanza sijabahatika kukutana na mwanake ambae mimi namtaka, nafikiri Mungu bado hajanipa huwaga nakutana na machizi, kwa sababu mimi sipendi, mwanamke aliyelelewa na kufundwa vizuri vitu vya ndani huwezi ukavitoa nje. 

Msanii DUDU BAYA
 Kwa mimi binafsi siongeagi  kwa wanaume wengine, napenda sana siri za familia zibaki kuwa siri za familia. Kwa mfano huyu jinsi alivyoenda kwenye media asitarajie nimtamrudia kabisa, ile tabia ya kwenda kwa jirani na kanga moja ikianguka? Kweli kabisa kicheni party zinaendelea lakini hazisaidii kitu chochote,” alisema

Zitto Kabwe ndani ya ulinzi Mkali

CHAMA cha Alliance Transparency For Change (ACT) Mkoa wa Kigoma, kimeahidi kumlinda na kumtetea Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), kutokana na changamoto zinazomkumba kupitia watu wachache wanaotaka kumwangusha kisiasa.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya chama hicho, Bw. Jaffar Kasisiko, aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Cine Atlas, kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji.
 
Alisema chama hicho hakipo tayari kuyafumbia macho matatizo yanayomkuta Bw. Kabwe na kumshauri mbunge huyo aachane na CHADEMA badala yake ajiunge na ACT ili aweze kukusanya wanachama kuanzia ngazi ya kitongoji, vijiji, kata na wilaya.
 
Aliongeza kuwa, uongozi wa CHADEMA una hila ya kusambaza maneno kwa umma dhidi ya Bw. Kabwe ili kulinda masilahi yao binafsi badala ya kutetea haki za wanyonge.
 
“Kabwe asipoteze muda wa kulumbana na uongozi wa CHADEMA, huu ni wakati mwafaka kwake kufanya uamuzi makini wa kwenda kuifuta kesi dhidi ya chama chake mahakamani na kujiunga na ACT,” alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Msafiri Wamalwa.
 
Katibu Mwenezi Wilaya ya Kigoma kutoka chama hicho, Anzoluni Kibela, alisema ACT imeandaa kadi kwa ajili ya Bw. Kabwe ambapo kuna wabunge 18 wapo tayari kujiunga na chama hicho kwenye uzinduzi rasmi ulipangwa kufanyika mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.
 
Naye Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. Shaban Mambo, aliwasihi wananchi wamuunge mkono Bw. Kabwe atakapojiunga na chama hicho ili aboreshe hali ya usafiri wa reli ya kati kwa kuwaletea treni inayotumia umeme kwa gharama zake.
 
Baadhi ya wanachama wapya wa ACT akiwemo aliyekuwa Mweka Hazina wa CHADEMA Kigoma Ujiji, Bw. Hamidu Hamis na Katibu wa ACT wilayani humo, Bw. Haji Idd, walisema wamejiunga na chama hicho ili kuleta uwazi  na  uwajibikaj

CCM yajipa mtihani


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
Kelele ambazo zimepazwa na watu wa kada mbalimbali nchini dhidi ya mchakato wa Katiba mpya zimeifanya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukutana kwa dharura, huku kukiwa na taarifa ndani ya chama hicho kuwa kuna hoja zinazokinzana juu ya kuendelea au kusitishwa kwa muda kwa Bunge Maalum la Katiba.

Kikao hicho kinachokutana mjini hapa leo, inadaiwa kitajadili miito ya wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa kauli za kumtaka Rais Jakaya Kikwete aliahirishe Bunge Maalum la Katiba linaloendelea na vikao vyake hadi hapo maridhiano yatakapopatikana baina ya CCM na wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Bunge hilo lililorejea katika ngwe ya pili Agosti 5, mwaka huu baada ya kuahirishwa Aprili 25, mwaka huu kupisha mkutano wa bajeti sasa linahudhuriwa na wajumbe wengi kutoka CCM, wachache kutoka kundi la 201 na wachache zaidi kutoka vyama vidogo vya siasa.

Wajumbe wengi wa vyama vinavyounda Ukawa vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walitoka nje ya Bunge hilo Aprili 16, mwaka huu wakilalamikia mambo mbalimbali ikiwamo Bunge hilo kuweka kando Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti  Jaji Mstaafu Joseph Warioba na kujadili rasimu mbadala ya CCM.

Wadau hao wanapendekeza kwamba Bunge hilo liahirishwe hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kumalizika.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya chama hicho, kimeeleza kuwa kikao hicho cha leo kilitanguliwa jana jioni na kikao kingine cha Sekretarieti ambacho hupanga ajenda zitakazojadiliwa.

“Baadhi ya viongozi wa juu, tayari wameshawasili akiwamo Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula ambaye alishinda jana kutwa nzima hapa ofisini akijaribu kuandaa mazingira, Pia nimemuona Nape Nnauye, lakini Rais Kikwete   ambaye ni Mwenyekiti wa CCM yeye ataingia kesho (leo) asubuhi kwa ndege…Na jioni hii (jana) tunampokea Katibu Mkuu (Abdurahaman Kinana),” kilisema chanzo hicho.

NIPASHE lilimshuhudia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwasili mjini hapa majira ya saa 8:36 mchana akitokea jijini Dar es Salaam na kukutana faragha na baadhi ya mawaziri katika ukumbi wa Mkapa.

Wajumbe wa kamati kuu waliotakiwa kuwa wamefika Dodoma kwa ajili ya kikao hicho ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wassira; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka; Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Pindi Chana.

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi; Dk. Salim Ahmed Salim,  Profesa Makame Mbarawa, Dk. Maua Daftari, Hadija Aboud  na Waziri wa Nchi, Ofisi Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa miito ya wadau inayotolewa hivi sasa kila kona ya nchi, ikimtaka  Rais Kikwete aliahirishe bunge hilo, imekuwa ikimpasua kichwa na kwamba kilichozungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema mwishoni mwa wiki iliyopita alisema ni maono ya serikali kukubaliana na wadau, lakini kwa sharti la kuwaanda kisaikolojia Watanzania.

“Zipo ajenda nyingine ambazo nadhani zitajadiliwa, lakini kubwa ni hoja zinazotolewa na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, shinikizo la vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutaka maridhiano na Rais Kikwete baada ya kususia Bunge Maalum la Katiba, kupokea taarifa ya Kamati ya Maadili ambayo ilipewa kazi ya kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada wake waliofungiwa kwa muda wa mwaka mmoja,” chanzo hicho kilisema.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa kutokana na joto la kisiasa kupanda hususani shinikizo la kutaka kutafutwa kwa maridhiano na kuahirishwa kwa Bunge hilo vinaweza kuwafanya CCM walegeze msimamo wa kuendelea na vikao vya Bunge Maalum.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipozungumza na NIPASHE jana jioni, alisema kwamba  ajenda ya kikao hicho ni kupokea taarifa ya maendeleo ya mchakato wa Bunge Maalum la Katiba.

Nape alisema kikao hicho ni mfululizo wa vikao vya Kamati Kuu na siyo cha dharura ila ni kamati maalum.

Nape aliongeza kuwa katika kikao hicho watapeana taarifa kuhusu mambo yanayoendelea katika Bunge Maalum la Katiba.
Nape alikanusha taarifa kwamba kikao hicho pia kitajadili suala la wanachama wake sita waliopewa dhabu ya mwaka mmoja kutojihusisha na shughuli za chama hicho na kuwa chini ya uangalizi kutokana na tuhuma kuwa walianza kufanya kampeni kabla ya muda rasmi kinyume cha kanuni na taratibu za CCM.

Wanachama hao waliochukuliwa hatua hiyo Februari mwaka huu ni mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Stephen Wassira; Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

“Wanaosema kuja ajenda kuhusu adhabu ni uzushi, ni maneno ya mitaani,” alisema Nape na kuongeza kuwa watu wasijenge hali ya wasiwasi na kwamba chama hicho kitatoa taarifa rasmi baada ya kikao hicho.

 

Subscribe to our Newsletter

Contact our Support

Email us: youremail@gmail.com

Our Team Memebers